DINI YA KISHETANI YA VUTA WATANZANIA WENGI
Makundi ya dini za waabudu shetani sasa yameamua kujiweka wazi na kutangaza hadharani jinsi ya kumuabudu shetani, hilo halina ubishi tena. Matangazo kwenye mitandao ya kijamii inawaalika watu kujiunga na kuwapa mbinu za kuwa waabudu shetani. Uchunguzi wa chanzo cha blog umebaini kuwa, baada ya aliyekuwa kiongozi wa dini hiyo, katika Wilaya ya kimasonary ya Africa Mashariki, Andy Chande, kuendesha mahojiano maalumu, katika kituo kimoja cha radio na kulipamba kundi la Freemason akidai ni chama cha hiari, mamia ya watanzania hasa vijana, wamekuwa wakihaha kujiunga na dini hiyo kwa kasi kubwa. Wakati Chande akidai kundi hilo sio la kidini, bali ni chama cha hiari mahojiano hayo yanatofautina sana na maelezo ya kina kuhusu kundi hilo, katika kitabu chake kiitwacho Shujaa katika Africa, Safari toka Bukene. Kwenye Uk. 169, wa kitabu hicho Chande anaeleza mwenyewe kuwa, miongoni mwa digree nyingi alizonazo kulingana na mafunzo aliyoyapata ndani ya kundi hilo, yakiwemo ya matambi