ULAJI WA KITIMOTO NI HATARI SANAA KWA AFYA YA BINADAMU
Kwa ufupi Hayo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni katika wilaya za Mbulu, Kongwa, Sumbawanga, Mpanda, Iringa, Urambo na Mbozi ambako walibaini kuwa ulaji wa nyama hiyo maarufu kama kitimoto ni hatari zaidi kwa afya ya binadamu. Dar es Salaam. Hatari! Watu wanaokula nyama ya nguruwe ambayo itakuwa haijaivishwa vizuri wako katika hatari ya kuambukizwa minyoo aina ya tegu na magonjwa mbalimbali ukiwamo wa kifafa. Hayo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni katika wilaya za Mbulu, Kongwa, Sumbawanga, Mpanda, Iringa, Urambo na Mbozi ambako walibaini kuwa ulaji wa nyama hiyo maarufu kama kitimoto ni hatari zaidi kwa afya ya binadamu. Kiongozi wa jopo la watafiti hao, Mhadhiri wa UDSM, Chacha Mwita alisema kati ya watu 1,036 waliofanyiwa vipimo, 150 walikutwa na maambukizi ya minyoo hiyo na kwamba walibaini kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa minyoo y