JITAMBUE,JITAFAKARI,CHUKUA HATUA & BADILI MAISHA YAKO!!

ukiona huna usemi na maisha yako,ulevi,uvutaji,ufuska,kundi rika,ufukara,unakataliwa na jamii,umetengwa,mipango haifanikiwa mara kwa mara,jua tayari uko kifungoni na katika hali hiyo kamwe hutaweza piga hatua maishani,usisite lazima ujifikie namna ya kutoka . maarifa ya namna ya kutoroka katika gereza hilo!!!Wake up!Your Comrade-Pius Mushi…Break Out Free!!!!!kikwazo kikubwa cha mafanikio ni wewe mwenyewe na vile uishivyo!!!-

Kuwa mtu zima haitokani tu umri wa mtu,kuwa mtu mzima ni hatua mtu anayofikia baada ya kujitadhimini na kuchukua hatua mhimu katika maisha ya mtu binafsi..ni uamuzi wako kukua au kubaki mtoto.
Sina shaka ya kwamba matatizo yaliyokuwa yakiniandama siku za nyuma yalikuwa ni mahususi kwangu tu,bali na hatua katika maisha na vijana wengi aidha wako kwenye hali hiyo ama wamekwisha ivuka au wanaelekea,
Hakuna kipindi kigumu kama ujana ,napenda kusema hivyo kwa sababu ni wakati ambao kijana anakutana na mambo angali maarifa yake ni duni.Makundi rika,pombe,madawa ya kulevya na sigara,umalaya,pesa na mengine mengi yote kwa pamoja yanamshambulia mtu mmoja asiye na maarifa ama mwenye maarifa duni.
Lengo hasa la kuandaa ukurasa huu,ni kutoa ushuhuda wangu binafsi kwa vijana wenzangu,juu ya changamoto na magumu yanayotukabili.Vyovyote vile hali yako ilivyo,aidha mbaya sana,nzuri kiasi au nzuri sana waweza piga hatua.Kwa wale wenzangu na mimi ambao hali zao sio shwari aidha kimahusiano katika jamii,kifedha na kiroho,napenda kukuhakikishia kuwa waweza toka hapo ulipo na kukaa mahali pazuri kama upo tayari kujitadhimini na kuchukua hatua sahihi.
Najaribu kuzungumzia mabadiliko,kama hauridhiki na hali uliyo nayo kwa sasa,msaada pekee uko kwako wewe mwenyewe,jisaidie kwanza wewe ndipo na wengine wakuone na kukusaidia pia.Kama ulikuwa haufahamu,ngoja nkufamishe rafiki ya kuwa,vijana wengi wako magerezani,sio keko wala segerea bali vifungo vya nafsi/soul.Niamini huweza piga hutua yeyote ya kuridhisha kama upo kifungoni.Aidha apo ulipo unatamani kuwa na biashara yako,kujiendeleza kitaaluma au vyovyote vile,hutaweza!!!hutaweza kwa nini?
Siri ya mafanikio kwa mtu yeyote awe kijana ama mtu mzima ni mabadiliko,mabadiliko yenye muelekeo wa kule unakotaka kwenda.Sasa basi jiulize,unaweza badilika?Mabadiliko sio rahisi,narudia kusema sio rahisi kabisa kubadilika,kwa sababu tayari upo kifungoni,na anayekushikilia,aidha ni bwana jela ulevi,madawa,ufukara,ufuska,kundi rika na wengineo ,hawako tayari kukubali wewe uende,niamini.
Nasema hivi kwa sababu zoezi la kubadili maisha nami nililipitia,na ugumu wake niliuona,ni hatari sana na ndio maana wengi wamezeekea gerezani,namaanisha wameishia kuwa wavuta sigara,pombe,uhuni,mafukara mpaka siku watakapo kufa,na utakapo kufa basi bwana jela ndipo atapo kuacha nduguzo wakakuzike.
Najua haujanisoma bado ya kuwa nataka kukueleza nini hasa,mtu yeyote aweza kuwa vile anavyotaka,aidha kiongozi,tajiri,msomi,mkulima hodari,mfugaji hodari,mpenwa na watu na hata jemedari bora kama tu ataweza,na kuamua kubadili maisha yake na kuyaweka katika uelekeo shahili wa kule anakotaka kuelekea,kazi nyingine muachie Allah,ukishashabadili maisha yako huitaji kusumbuka zaidi ya hapo,mafanikio sio kazi yako bali ni matokeo yatakayo kufuata.
Mabadiliko yana matokea,na matokeo ni automatic,huyapangi wewe yatajitokeza yenyewe,ndio maana ya matokea.Chakusumbukia wewe ni mabadiliko/Change.
Shida kubwa iko hapa,kubadilika!!unaweza??kama huwezi,jiulize kwa nini?
A.Sababu ya ulevi.
B.uvutaji
C.uvivu
D.ufuska
E.hali duni ya maisha/ufukara.
Sasa nikupe siri ndugu yangu,vifungo vyetu vinatofautiana,wengine tumefungwa maisha,wengine wako kwenye vifungo vya mda, wengine kifungo cha nje ,kwa wale wezangu namimi tuliofungwa maisha na kweli tunahitaji kufunguliwa,siri ni moja tu,tunatakiwa kufa ili bwana jela atuachie kisha tufufuke tena tukiwa huru uraiani.Umenielewa kweli?.Namaanisha kuikana nafsi uliyo nayo sasa/kufa/beba msalaba/mateso ambayo ndio kifungo chenyewe na kuishi maisha mapya bila nafsi hiyo chafu.
Namaanisha utakapoamua kubadilika,haitakuwa rahisi,utaumia sana,na uvumilivu ni mkubwa  unahitajika ili ubadilike,kama unafikiri ni rahisi kuacha sigara waulize wavutaji ni mara ngapi wamejaribu na kutoka patupu au kitu chochote kingine ulichokwisha zoea
Kikwazo cha maendelo yako,ni wewe mwenyewe,aidha tamaa imekuzidi mpaka njia huoni,haujiamini,utegemezi na mengine mengi.Kujitakasa ndio njia pekee itakayo kupa nguvu na mwangaza wa wewe kubadilika.
“Nilikuwa natamani maisha bora sana lakini nilishindwa,ila nilipodali maisha yangu,ghafla mambo yakaanza ninyookea ,siamini kwa hatua niliyofikia,na ninajiogopa maana nimekuwa nikipanda juu kila kukicha,sikuombewa,nilijitadhimini nikaona niapokosea,nikarudi kwenye mstari,na sasa kila kitu ni mdebwedo kwangu”.
Nakutaadharisha,kubadili maisha sio rahisi,na wengi hawataweza,kama utaweza achana na maisha yako ya zamani,basi wewe ni askari bora.Basi Ndugu kama utafika mahala na kuamua badili maisha yako,kumbuka hili”ni uamuzi wako binafsi,na usifanye makosa kwa kutangaza kwa mtu au rafiki,huo ni msalaba wako,beba mwenyewe,na Mungu atakusaidia…
Utajuaje yakupasa kubadilika??ukiona humiliki maisha yako,yaani huna control ya maisha yako,aidha ulevu unakuendesha,ufukara unakuendesha,umalaya unakuendesha,kundi rika linakuendesha,tamaa mbalimbali zinakuendesha,huna usemi juu ya maisha yako:Jua tayari uko kifungoni,na amini nakuambia,katika hiyo hali hutaweza fanikiwa maana uko gerezani tayari,kama wewe kweli ni shujaa unatakiwa utoroke”kama mimi ndipo utapata dira.



Comments

Popular posts from this blog

THE FRACTURE AND SPLINTING

BEST WAYS TO TAKE BLOOD PRESSURE

KUNA VIUMBE WA AJABU WANAOISHI ANGANI!